The SAINT Pictures in this gallery come from a variety of sources,but most of them are from modern Roman Catholic "holy cards." Some of the images are great art, but it is important to understand that the point of an image of saint for the believer has nothing to do with art. Understandings of images and how they relate to the person they portray has certainly varied, but "art" has raely been the goal. The believer, rather, wants a reminder of a connection with the saint, and in many cases the saint's presence is actualized through the image.

SALA KWA MALAIKA WAKO MLINZI.

Sali kila siku unapoamka na kabla hujalala,ATUKUZWE 7 kwa heshima ya malaika wako mlinzi,kisha sali;

Malaika wa Mungu mlinzi wangu mpenzi, ambaye upendo wake unanifanya niwepo hapa uwe nami leo hii,kuniangaza na kunilinda,kunitawala na kuniongoza, AMINA.

SALA KWA MT. MIKAELI MALAIKA MKUU

MTAKATIFU MIKAELI MALAIKA MKUU,utulinde katika vita,uwe kinga yetukatika maovu na maoteo ya shetani,Mungu amtiishe tunaomba sana,nawe Mkuu wa Majeshi ya Mbinguni,kwa nguvu ya Mungu,uwaangushe motoni shetani na pepo wabaya wengine wote,wanaozunguka duniani,ili kuzipoteza roho za watu. AMINA.
KUMBUKA KWA MTAKATIFU YOSEFU
Kumbuka Ee mchumba safi wa Bikira Maria/hujasikika hata mara moja/kwamba umemwacha mtu aliyeomba msaada wako./ Kwa matumaini hayo ninakukimbilia wewe,/na kuomba ulinzi wako./Ee Baba Mlishi wa Mkombozi,/usikatae ombi langu nyenyekevu,/bali kwa wema wako unisikilize na unijibu.
AMINA.
SALA KWA MT. ANNA.
(kwa kupata fadhila ya pekee).
MTUKUFU Mt.Ana,uliyejawa huruma kwa waote wakuombao,na upendo kwa wale watesekao,nikielemewa na uzito wa matatizo yangu,ninajitupa miguuni pako na kukuomba unisaidie haja yangu ninayoileta kwako chini ya ukingaji wako wa pekee.
Upende kuifikisha kwa binti yako Bikira Maria na kuiweka mbele ya kiti cha enzi cha Yesu,ili apate kuikubali.Usiache kuniombea hadi ombi langu litakapokubaliwa.Juu ya yote unipatie neema ya kumtazama siku moja Mungu uso kwa uso,nami pamoja nawe na Maria na watakatifu wote tumsifu na kumtukuza kwa milele yote.
Ee mwema Mt. Ana, mama wa yule aliye uzima,tulizo na matumaini yetu,utuombee na kutupatia ombi letu.(x3).
WARIDI LA SALA YA NOVENA
Ee Mtakatifu Teresia mdogo wa Mtoto Yesu,nakuomba unichumie waridi kutoka kwenye bustani ya Mbinguni ne unitumie kama ujumbe wa upendo.Ewe waridi dogo la Yesu,umwombe Mungu anijalie neema hii ninayoiweka mikononi mwako...(taja ombi lako)
Mt.Teresia,kama wewe,unisaidie mimi pia niuamini upendo wa Mungu kwangu,ili kila siku niingie "Njia yako ndogo".
AMINA.
SALA YA MT.FRANSISKO
WA ASSISSI

Ee Bwna unifanye kuwa chombo cha amani.Palipo chuki unifanye nieneze mapendo.Palipo na mashaka pawe na amani.Palipo na tuamini pawe na matumaini.Palipo na giza pawe na mwanga. Palipo na huzuni pawe na furaha.

Ee Bwana Mungu,unijalie nisitafute kufarijiwa,bali kufariji,kupendwa bali kupenda, kwani ni kwa kutoa ndipo tunapokea,ni kwa kusamehe ndipo tunasamehewa na ni kwa kufa ndipo tunapoKea uzima wa Milele.
AMINA.

SALA ILIYOKUTWA KWENYE KABURI LA YESU 1503 AD.

Ee Mungu mwenyezi uliyekufa msalabani kwa ajili ya dhambi zangi,uwe nami. Msalaba Mtakatifu wa Yesu-unihurumie.
Msalaba Mtakatifu wa Yesu-uwe mkingaji wanguMsalaba Mtakatifu wa Yesu-uniondolee maovu yote.
Msalaba Mtakatifu wa Yesu-uniondolee maumivu yote.
Msalaba Mtakatifu wa Yesu-unifanye niende kwenye wokovu.

Unikinge na ajali za mwili,uniondolee hatari ya kifo cha ghafla.Nauabudu msalaba mtakatifu wa Yesu Kristu wa Nazareti uliyesulibiwa,unihurumie,unifanye niweze kuondokana na Roho ya uovu wakati wote,ee mama wa msaada wa daima,naja mbele ya picha yako takatifu, na kuomba msaada wako kama mtoto.Jionyeshe sasa kwangu kwamba u mama unionee huruma. Ee mama mpenzi wa msaada wa daima,kwa ajili ya upendo uliokuwa nao kwa Yesu na kwa heshima ya majeraha yake matakatifu,unisaidie haja yangu......(taja).
Ee mama mpendevu,ninayaacha yote kwako kwa Jina la Baba,ninayaacha yote kwako kwa Jina la |Mwana,ninayaacha yote kwako kwa Jina la Roho Mtakatifu.Amina.
BIBI YETU WA MSAADA WA DAIMA,UTUOMBEE(mara tatu).

SALA KWA MTAKATIFU YUDA.

Ee Mtakatifu Yuda,mtume na shahidi,uliye mkuu katika fadhila natajiri wa miujiza,jamaa wa karibu wa Yesu Kristo,mwombezi mwaminifu wa wale wote waombao msaada wako nyakati za shida.Ninakukimbilia wewe na kukusihi unisaidie,wewe uliyepewa uwezo mkubwa na Mungu. Unisaidie katika shida yangu hii....(Taja ombi lako).
Nami ninaahidi kukufanya ili ujulikane na watu wakuombe.
(sali)Baba yetu tatu,Saalamu Maria tatu na atukuzwe tatu.
Mtakatifu Yuda,utuombee wote tuombao msaada wako.Amina.
SALA KWA MTAKATIFU YOSEFU,YENYE MIAKA ZAIDI YA 1900.

EE MTAKATIFU YOSEFU,ambaye ulinzi wako ni mkubwa na wa haraka mbele ya kiti cha enzi cha Mungu,ninakukabidhi nia na haja zangu zote. EE MT.YOSEFU,unisaidie kwa aombezi yako yenye nguvu,na unipatie kutoka kwa mwanao Mungu,Baraka zote za kiroho,kwa njia ya Kristu Bwana wetu,ili nikishapata msaada wako wa mbinguni ningali haspa duniani niweze nami kumsifu,kumwabudu na kumshukuru Mungu aliye Baba mwema kabisa kushinda wote.EE MT.YOSEFU,sichoki kamwe kufikiri moyoni kwa upendo jinsi Mtoto Yesu alivyokuwa amesinzia mikononi mwako.Akiwa amepumzika hivyo karibu na moyo wako, sithubutu kujongea,nisije nikamsumbua,bali nakuomba wewe umkumbatie na kumbusu kwa niaba yangu na kumwambia anipe busu lake nitakapovuta pumzi yangu ya mwisho.MT.YOSEFU msimamizi wa wenye kuzimia Roho,utuombee.Amina.